Proverbs 30:1-4

Misemo Ya Aguri

1 aMisemo ya Aguri mwana wa Yake, usia: Huyu mtu alimwambia Ithieli,
naam, kwa Ithieli na kwa Ukali:


2 b“Mimi ni mjinga kuliko wanadamu wote;
sina ufahamu wa kibinadamu.

3 cSijajifunza hekima,
wala sina maarifa ya kumjua yeye Aliye Mtakatifu.

4 dNi nani ameshapanda mbinguni na kushuka?
Ni nani ameshakusanya upepo
kwenye vitanga vya mikono yake?
Ni nani ameshafungia maji kwenye nguo yake?
Ni nani ameimarisha miisho yote ya dunia?
Jina lake ni nani, na mwanawe anaitwa nani?
Niambie kama unajua!

Copyright information for SwhKC